Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

Miradi Yetu

SHIRIKA LINAMILIKI MIRADI YAKE YENYEWE IFUATAYO

1, MRADI WA MAKAA YA MAWE KABULO - KIWIRA

Shirika linamilika leseni za uchimbaji wa makaa ya mawe iliyopo Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe yenye mashapo zaidi ya tani milioni 85. Kwa sasa uchimbaji, uchakataji, na uuzaji wa makaa ya mawe wa wingi (massive coal mining) unaendelea mgodini.

2. MRADI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA ( RAFIKI BRIQUETTES)

Shirika limeanza uzalishaji wa Nishati safi ya kupikia inayoitwa Rafiki Briquettes kama chanzo cha Nishati safi kwa kutumia makaa ya mawe yanayopatikana katika leseni za Shirika. Shirika lilikamilisha usimikaji wa mitambo miwili mikubwa yenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa na kuanza uzalishaji wa Nishati hiyo katika maeneo ya Kisarawe Mkoa wa Pwani na Kiwira Mkoa wa Songwe. Kwa sasa, Shirika linaendelea na usimikaji wa mitambo mingine miwili katika Mikoa ya Dodoma na Tabora. Aidha, Shirika linatarajia kusimika mtambo mwingine katika Mkoa wa Geita.

3. MRADI WA HUDUMA ZA UCHORONGAJI

Shirika limeendelea na kandarasi za uchorongaji kwenye migodi ya madini katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Shanta Singida, Chunya. Aidha, Shirika limefanya uwekezaji katika mradi huu ukihusisha mitambo ya kisasa ya uchorongaji, low bed, magari pamoja na vifaa saidizi mbalimbambali. Kati ya mitambo iliyonunuliwa na Shirika ipo mitambo mikubwa ya kisasa ya uchorongaji ikiwa ni pamoja na Drilling Rig Multipower na deep hole drilling rig ambazo zimeongeza ufanisi zaidi katika shughuli za uchorongaji.

4. MRADI WA KOKOTO CHIGONGWE

Shirika linamiliki leseni 10 za Kokoto katika eneo la Chigongwe Mkoani Dodoma. Shirika limesimika mtambo wenye uwezo wa kusaga Kokoto tani 150 hadi 200 kwa saa katika eneo hilo na uzalishaji ulianza Julai 2024.

5. MRADI WA KUUZA KEMIKALI NA VILIPUZI

Shirika lina mradi wa Biashara ya kuuza vilipuzi na kemikali kwenye vituo vya mfano vya Lwamgasa, Katente, Nyakafuru na Itumbi na katika mmgodi wa STAMIGOLD. Aidha, Shirika linategemea kuanza kuuza kemikali na vilipuzi katika migodi mingine ya kati na mikubwa nchini ili kuongeza wigo wa wateja na kusogeza huduma hiyo karibu na wachimbaji.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo