Miradi ya Ubia
KAMPUNI ZA UBIA
Kampuni ambazo zimeanzishwa kwa ushirikiano kati ya Shirika na Wawekezaji. Kila mbia huchangia rasilimali kama mtaji, utaalamu au masoko ili kuwezesha kuanzisha na kuendesha mradi husika. Faida, hasara na viashiria hatarishi vya mradi husika hugawanywa kulingana na makubaliano. Hadi sasa, Shirika lina miradi mitatu ya Ubia ambayo ni Kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza, mradi wa Buckreef na mradi wa Nikel wa Ntaka.
1. KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU MWANZA
Kiwanda cha kusafisha Dhahabu Mwanza kinamilikiwa na STAMICO kwa asilimia 25 na wabia wenza Kampuni ya Goodfield International DMCC ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Dubai), kwa asilimia 75. Kina uwezo wa kusafisha kilo 480 za Dhahabu kwa siku kwa kiwango cha Kimataifa cha asilimia 99.99.
2. MGODI WA DHAHABU WA BUCKREEF
Mradi wa Dhahabu wa Buckreef unamilikiwa na STAMICO kwa hisa asilimia 45 na Tanzania American International Development Corporation 2000 (TANZAM 2000) kwa hisa asilimia 55. Mradi huu unahusisha uchimbaji na uuzaji Dhahabu.
3. MRADI WA UCHIMBAJI MADINI YA NIKELI - NTAKA
Shirika linamiliki kwa ubia mradi wa uchimbaji madini ya Nikeli uliopo Ntaka Mkoa wa Lindi na Kampuni ya Coastal Nickel Industry ya nchini China. Mradi huu unahusisha uchimbaji na uchenjuaji madini ya Nickel.