Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

STAMICO YAINGIA MKATABA WA UCHORONGAJI WENYE THAMANI YA SHILLINGI MILIION 700

Imewekwa: 11 March, 2025
STAMICO YAINGIA MKATABA WA UCHORONGAJI WENYE THAMANI YA SHILLINGI MILIION 700

Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO), Leo tarehe 11/09/2023 limesaini kandarasi ya Uchorongaji na kampuni ya FUXING RESOURCE LTD kutoka Nchini China.

Mkataba huo wa uchorongaji umesainiwa jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mtandaji Bw. Deusdedith Magala na Mkurugenzi wa Kampuni ya FUXING RESOURCE LTD Bw.LIU LIAN QUAN

Kandarasi hiyo ya uchorongaji yenye thamani ya shilingi million 700 ina jumla ya mita 3000 kwa njia ya RC.

Kazi ya uchorongaji itafanyika eneo la Magambua Wilayani Chemba Mkoani Dodoma kwa ajili ya utafiti wa Madini ya LITHIUM.

Aidha kazi hiyo ya Uchorongaji inategemea kuanza tarehe 25/09/2023.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo