Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA PIC YATEMBELEA MGODI WA STAMIGOLD

Imewekwa: 11 March, 2025
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA PIC YATEMBELEA MGODI WA STAMIGOLD

Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imetembelea Mgodi wa STAMIGOLD tarehe 21 Februari, 2024 na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi.

Ziara hii ni muendelezo wa ziara ya Kamati hii katika miradi ya STAMICO

Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake Ndugu Deus Clement Sangu imeona maendeleo mazuri ya uendeshaji wa shughuli za mgodi na kupongeza hatua mbalimbali za utekelezaji zikiwemo mgodi huo kuunganishwa na umeme wa gridi ya taifa wa TANESCO ambao umesaidia kupunguza gharama

Meneja Mkuu wa mgodi Ndugu Ali Ali aliielezea kamati shughuli mbalimbali za mgodi Ikiwemo mafanikio mbalimbali pamoja na kuwaongoza wajumbe kutembelea maeneo ya mgodi

Aidha ,Katika kufunga ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya STAMIGOLD Bi Rehema Mwakajube ameishukuru kamati kwa maelekezo yake na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo hayo.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo