Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA STAMICO KWA UWEKEZAJI WA NISHATI YA KUPIKIA YA RAFIKI BRIQUETTES

Imewekwa: 14 March, 2025
KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA STAMICO KWA UWEKEZAJI WA NISHATI YA KUPIKIA YA RAFIKI BRIQUETTES

Kamati ya NISHATI na MADINI wakiongozwa na Mwenyekiti  Mh. Dkt.David Mathayo (MB) leo tarehe 13 Machi walifanya ziara kwenye mradi wa kutengeneza nishati mbadala  ya Rafiki Briquettes.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO,  Dkt. Venance Mwasse aliwaongoza wajumbe wa kamati kushuhudia shughuli  mbalimbali zinazofanyika katika uzalishaji nishati ya Rafiki Briquettes  zikiwemo 
Uchomaji wa nyama , mahindi ya kuchoma na upikaji wa maharage.

Wajumbe wa Kamati  walipongeza mageuzi na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Shirika katika mgodi wa Kiwira na Rafiki Briquettes kwa ujumla. 

Wajumbe  pia waliridhishwa na maendeleo ya mradi wa nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquette  na kusisitiza nishati hiyo  muhimu iweze kuwafikia  wananchi wengi  ili kuendelee kuunga mkono ajenda ya  upatikanaji wa nishati safi na nafuu kwa Watanzania wote.

Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri wa Madini, Dkt Steven Kiruswa  ambae aliambatana na Kamati katika ziara hiyo aliishukuru kamati kwa maoni yao na miongozo mbalimbali wanayoitoa kwa Shirika ambayo imeleta mafanikio makubwa katika mradi wa Rafiki Briquettes kuanzia utafiti wake hadi kwenye uzalishaji.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo