Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAWEKA HISTORIA, YAPIGILIA NYUNDO MAELEKEZO YA RAIS SAMIA UJENZI WA KIWANDA CHA CHUMVI LINDI


▪️ *Waziri Mavunde aimwagia Sifa STAMICO kwa utekelezaji wa 4R*.

▪️*RC Lindi ashangilia maendeleo ya wachimbaji wa chumvi kupitia kiwanda cha STAMICO*

▪️*Dkt. Mwasse akazia Dhamira ya Serikali katika kuwawezesha Wachimbaji Wadogo kupitia STAMICO*

▪️*M/Bodi ya STAMICO asisitiza kiwanda kuanza kutema chumvi April, 2025*

Mnamo tarehe 18 Septemba, 2024 STAMICO imepokea rasmi *Hati ya umiliki wa Ardhi* katika wilaya ya Kilwa ambapo ni rasmi sasa eneo hilo litatumika katika kutimiza adhima ya *Mhe. Dkt. Samia Suluhu* Rais Samia ya ujenzi wa kiwanda cha Chumvi kinachosimamiwa na STAMICO.

Aidha, *Mhe. Anthony Mavunde* Waziri wa Madini Tanzania ameipongeza STAMICO kwa kutekeleza ahadi yake juu ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Chumvi Mkoani Lindi.

*Katika tukio hilo* Mhe. Waziri amepokea hati ya umiliki wa ardhi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi ikiwa ni hatua muhimi katika kuanza ujenzi rasmi.

Katika hatua nyingine Waziri Mavunde ameongeza kwa kusema kuwa anajivunia kuwa na wasaidizi wawili wenye weledi na maono, ambao ni Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Jenerali (mstaafu) Michael Isamhuyo na Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Dkt. Venance Mwasse.

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linaenda kuweka historia ya kipekee katika Mkoa wa Lindi kwa kubadilisha maisha ya wachimbaji wa Madini chumvi .

Katika hotuba yake ya kukabidhi site Waziri Mavunde amewataka wachimbaji hao kutumia fursa hii kushirikiana na Shirika hasa katika swala la kukuza mitaji, kuongeza thamani na kukuza masoko ya ndani na nje kwa bidhaa hii bora itakayozalishwa na STAMICO.

Chumvi itakayozalishwa na kiwanda itakuwa na ubora wa asilimia 99.5%.

*Akitoa Salam za Mkoa*, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu R. Telack ameipongeza STAMICO kwa kwa kuamua kuweka kiwanda mkoani Lindi kwani kitaendea kuinua Maisha ya wachimbaji wa madini ya chumivi ambao walikuwa wanateseka kwa kukosa soko la chumvi wanayozalisha.

Naye Mkurugenzi Mtendaji (STAMICO) *Dkt. Venance Mwasse* ameeleza wazi kuwa chimbuko la mradi huu ni mpango wa Shirika na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba kiwanda hiki kijengwe ili kiwasaidie wananchi wa Lindi na wazalishaji wa Chumvi,

Akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi Dkt. Mwasse alisema Shirika tayari limekwisha agiza Mtambo wa kusafisha na kuchakata Chumvi mpaka kwa asilimia 99.5% kutoka nchini India na unatarajiwa kuwasili mwezi Oktoba, 2024.

Aidha shughuli za ujenzi wa miundombinu ya Kiwanda unaanza mara moja.

*Kwa upande wake* Mwenyekiti wa Bodi (STAMICO) amesema katika juhudi hizo zote inatazamiwa kiwanda hicho kukamilika ujenzi wake mnamo Aprili, 2025 na kuanza shughuli hizo za uzalishaji wa Chumvi kwa haraka iwezekanavyo ili wananchi waanze kunufaika na shughuli zao za uchimbaji na uandaaji wa chumvi.

_Zifuatazo ni baadhi ya picha za Matukio_