News
ZIARA YA MD STAMICO YAPAISHA AGENDA YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI NA SALAMA YA RAFIKI BRIQUETTES KWA MAGEREZA ZANZIBAR
Leo tarehe 16 Desemba 2024 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa Dr.Venance Mwasse amefanya mkutano na Dr. Islam Salum Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar pamoja na mambo mengine wamejadili namna wanavyoweza kuisaidia jamii visiwani Zanzibar kufikiwa na nishati kupikia ya Rafiki Briquettes kwa kuzingatia sasa nchi inategemea kupiga marufuku uzalishaji wa kuni na mkaa na utekelezaji wa Sera ya nishati safi na salama.
Sambamba na mkutano huo katika kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi na salama ya kupikia Mkurugenzi wa STAMICO amefanya mazungumzo na ndugu Khamis Khamis Kamishina wa Magereza Zanzibar ili kufanikiza azima yao yakuachana na matumizi ya kuni na kutumia nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes.
Kwa upande wake kamishina wa magereza ameishukuru STAMICO na Mkurugenzi Mtendaji kufika ofisini kwake na kuonesha nia kuisaidia magereza kuhamia katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquettes na kuahidi kutekeleza yote yaliyoelezwa. Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt.Venance Mwasse alikuwa Zanzibar kufuatia mualiko wa Katibu Mkuu.