News
STAMICO YATANGAZA NEEMA KWA WACHIMBAJI WA MADINI NA WAZALISHAJI WA CHUMVI
Leo tarehe 11 Juni 2025, Kumefanyika uzinduzi wa Maonesho ya Madini na uwekezaji Mkoani Lindi katika Wilaya ya Ruangwa
Maonesho yamefunguliwa na Mgeni rasmi Mh Shaib Hassan Kaduara, Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar
Awali akitoa salamu za Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Venance Mwasse alisema Shirika katika Maonesho haya limekuja na fursa tatu;
*Fursa ya kwanza* Nishati safi ya Rafiki Briquettes kwa Wananchi wa Mikoa ya kusini na kuwasihi kutembelea banda la STAMICO kujifunza na kupata maelezo toka kwa wataalum juu ya *Nishati hii safi* ya *Rafiki Briquettes* ikiwa pamoja na kuwa Mawakala wa Nishati hiyo.
*Fursa ya Pili* ni Ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata chumvi kinachojengwa katika Wilaya ya Kilwa na kuwa Mkombozi kwa Wazalishaji wa chumvi kwa Mikoa ya Kusini. Fursa hii inaambatana na Mafunzo kwa wazalishaji wa chumvi itakayotolewa tarehe 12 Juni 2025.
Aidha Dkt Mwasse alielezea *Fursa ya Tatu* ni uwepo wa Mitambo mipya Kumi ya uchorongaji inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni Jijini Dodoma na kuwaalika wadau wote wa Sekta ya Madini kuhudhuria Uzinduzi.
Akiwasilisha salamu za Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack aliipongeza STAMICO kwa juhudi mbalimbali za kuwalea na kuwaendeleza Wachimbaji wa Wadogo nchini Wakiwemo wa Lindi.
Maonesho haya ambayo yamefunguliwa leo tarehe 11 Juni 2025 yanaudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 14 juni 2025.