News
AGENDA YA NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES YABEBWA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM NCHI NZIMA”CPA DKT.MWASSE
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan rasmi ameahirisha Mkutano Mkuu wa Chama uliodumu kwa siku Mbili kuanzia tarehe 18-19/01/2025 katika Ukumbi wa Jakaya Convection Center Dodoma. Katika mkutano huo pia yamefanyika Maonesho makubwa yaliyokusanya Wajumbe na wadau mbalimbali .
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) CPA Dkt. Venance Mwasse amechukua fursa hiyo kushukuru Uongozi wa CCM kwa kuandaa Maonesho hayo makubwa yaliyowakusanya watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya nchini na kupata fursa ya kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya Nishati Safi (Rafiki Briquettes).
STAMICO imetumia fursa hiyo kuinadi Nishati Safi ya Rafiki Briquettes kwa Wajumbe mbalimbali waliofika katika Banda la STAMICO ambapo imetumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wajumbe hao na watu mbalimbali.
Pia, katika Maonesho hayo STAMICO ilifanya live demonstration cooking kwa kutumia nishati ya Rafiki Briquettes Kupitia Wakala wake wa Rafiki Briquettes mkoa wa Dodoma kikundi cha Wanawake na Samia.